Utangulizi na Sababu ya Kuwepo:

Ilianzishwa mnamo Oktoba 25, 2008 kwa mpango wa vijana (hasa wanawake) wa Kivu, La Floraison ni shirika lisilo la faida la Kongo ambalo linafanya kazi kwa ajili ya ulinzi na kukuza haki za wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo hatarini yaliyoathiriwa na migogoro ya silaha, majanga ya asili na migogoro ya kiafya.

Dira, Utume na Maadili:

Utume (Mission): Katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika, La Floraison Asbl inaimarisha ustahimilivu na ushirikishwaji wa jamii zinazokabiliwa na majanga ya kibinadamu na mabadiliko ya hali ya hewa, kwa kipaumbele kwa uwezeshaji wa wanawake vijana na ulinzi wa watoto.

 

Maono (Vision): Jamii zenye haki, amani na ustahimilivu ambapo kila mtu anaishi kwa hadhi na kutumia haki zake kikamilifu.

 

Maadili: Utu (Humanity), Hadhi (Dignity), Usawa (Equity), Uwajibikaji (Accountability), Ufeministi (Feminism).

  

 

 

Utawala na Usimamizi wa Shirika

La Floraison ina mfumo wa utawala ulio wazi, shirikishi na unaozingatia mfumo wa kisheria wa kitaifa pamoja na kanuni za utawala bora za mashirika ya kibinadamu.

Mkutano Mkuu (Assemblée Générale) ni chombo cha juu kabisa cha kufanya maamuzi; huweka mwelekeo wa kimkakati, hupitisha sera za ndani, huidhinisha mipango na bajeti, na huchagua wajumbe wa Kamati ya Uongozi.

Tume ya Udhibiti (Commission de Contrôle) inahakikisha utekelezaji sahihi wa maamuzi ya Mkutano Mkuu na Kamati ya Uongozi, inakagua uzingatiaji wa taratibu za kifedha na kisheria, na inahakikisha uwazi na uwajibikaji katika shughuli za shirika.

Kamati ya Uongozi (CD) inasimamia mwelekeo wa kimkakati na usimamizi wa jumla wa shirika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi anawakilisha La Floraison kisheria katika shughuli zote za kiraia na anahakikisha utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano Mkuu.

Uhongozi wa utendaji (Direction Exécutive – DE) ni chombo cha utekelezaji cha La Floraison.

Mkurugenzi Mtendaji anawajibika kwa usimamizi wa kila siku wa shirika, ufuatiliaji wa shughuli, uhamasishaji wa rasilimali na usimamizi wa wafanyakazi.

 

 

Hadhi ya kisheria na utambuzi  

La Floraison inatambuliwa kisheria kwa mujibu wa Sheria Na. 004/2001 ya tarehe 20 Julai 2001 kuhusu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yenye Hadhi ya Kisheria (ASBL) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC).